Fasihi ya Kiswahili

Kitabu kiliandikwa na Shaaban Robert aliyekuwa "baba wa fasihi ya Kiswahili".

Fasihi ya Kiswahili ni fasihi ambayo huandikwa kwa lugha ya Kiswahili, hasa na watu wa Afrika Mashariki. Fasihi ya Kiswahili ni sehemu ya fasihi ya Kiafrika na fasihi ya Kibantu.

Mwandishi wa kwanza wa Kiswahili alikuwa Fumo Liyongo kutoka kisiwa cha Lamu (leo nchini Kenya) kati ya karne ya 9 na karne ya 10. Fumo Liyongo aliandika kwa Kingozi kilicho lahaja ya Kiswahili. Fumo Liyongo aliandika mashairi mengi kama "Sifa la Uta", "Utungo wa Ndoto" au "Wimbo wa Mapenzi".

Kitabu cha kwanza kilichogundulika kilikuwa Hamziya kwa mujibu wa Jan Knappert.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search